Maelezo ya Chini
b Mahali patakatifu palikuwa ni hema kubwa la kukutania lenye umbo la mstatili (rectangle), lililoshikiliwa kwa viunzi vya mbao. Hata hivyo, hema hilo lilikuwa limetengenezwa kwa vitu bora sana, yaani, ngozi ya sili, vitambaa vilivyopambwa vizuri, na mbao za bei ya juu zilizofunikwa kwa fedha na dhahabu. Mahali hapo patakatifu palizungukwa na ua. Ndani ya ua huo palikuwa pia na madhabahu yenye kupendeza ya kutolea dhabihu. Baadaye, yaelekea vyumba vingine vilivyotumiwa na makuhani vilijengwa kandokando ya hema hilo. Huenda Samweli alilala ndani ya mojawapo ya vyumba hivyo.