Maelezo ya Chini
a Huenda tarehe hii isilingane na ile ya Pasaka inayofuatwa na Wayahudi leo. Kwa nini? Wayahudi wengi leo wanaadhimisha Pasaka katika Nisani 15, wakiamini kwamba amri ile inayopatikana katika Kutoka 12:6 inaelekeza katika tarehe hiyo. (Ona gazeti la Mnara wa Mlinzi la Februari 15, 1990, ukurasa wa 14.) Lakini Yesu aliadhimisha Pasaka katika Nisani 14 kama ilivyoelekezwa katika Sheria ya Musa. Kwa habari zaidi kuhusu jinsi ya kufanya hesabu hiyo, ona gazeti la Mnara wa Mlinzi la Kiingereza la Juni 15, 1977 (15/6/1977), ukurasa wa 383-384.