Maelezo ya Chini
e Mnamo Novemba 22, 2010 (22/11/2010), kikundi cha mahakimu watano wa Baraza Kuu la Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu kilikataa ombi la Urusi la kutaka kesi hiyo ipelekwe katika Baraza Kuu la Mahakama hiyo. Walipokataa ombi hilo, walionyesha kwamba uamuzi wa Juni 10, 2010, ulikuwa wa mwisho na hivyo unapaswa kutekelezwa.