Maelezo ya Chini
a Namna gani ikiwa kijusi kinachokua tumboni kinaonekana kuwa na kasoro au viini-tete kadhaa vimepandikizwa tumboni? Kuua vijusi hivyo kimakusudi ni kutoa mimba. Ni jambo la kawaida kupata mimba za mapacha (wawili, watatu, au zaidi) unapotumia mbinu ya IVF, na hilo huongeza hatari kama vile mama kujifungua kabla ya wakati na kuvuja damu nyingi. Mwanamke aliyebeba vijusi vingi tumboni anaweza kuambiwa “achague vijusi vinavyofaa,” ili kijusi kimoja au kadhaa viuawe. Huo utakuwa utoaji mimba wa kukusudia, ambao ni sawa na kuua.—Kut. 21:22, 23; Zab. 139:16.