Maelezo ya Chini
b Wataalamu wa vitu vya kale wamefukua piramidi kadhaa, minara ya hekalu yenye ngazi karibu na Shinari. Biblia inasema kwamba wajenzi wa mnara wa Babeli hawakutumia mawe bali walitumia matofali na lami kama saruji. (Mwanzo 11:3, 4) Huko Mesopotamia, “ilikuwa vigumu kupata mawe,” kinasema kitabu The New Encyclopædia Britannica, ingawa lami ilipatikana kwa wingi.