Maelezo ya Chini
b Wamisri wa kale walitengeneza zaidi ya aina 90 za mikate na keki. Kwa hiyo, mkuu wa waokaji wa Farao alikuwa mtu maarufu. Naye mkuu wa wanyweshaji ndiye aliyesimamia kikundi cha watumishi ambao walihakikisha kwamba divai na huenda hata bia ambayo Farao alikunywa ilikuwa na ubora wa kiwango cha juu. Pia, walihakikisha kwamba vinywaji hivyo vilihifadhiwa vizuri ili mtu yeyote asije akavitia sumu, kwani njama kama hizo zilizokusudiwa kumuua mfalme zilikuwa zikitendeka katika makao ya wafalme. Basi haishangazi kwamba mkuu wa wanyweshaji angeweza kuwa mshauri aliyeaminiwa sana na mfalme.