Maelezo ya Chini
a Cerebral Palsy (CP) ni aina fulani ya ugonjwa wa kupooza kwa ubongo unaofanya mtu ashindwe kutembea au hata kusonga. Ugonjwa huo unaweza kumfanya mtu aanguke ni kana kwamba ana kifafa, apate matatizo ya kula, na ashindwe kuzungumza vizuri. Ugonjwa wa kupooza ubongo unaoitwa Spastic quadriplegia ndio mbaya zaidi kati ya magonjwa yote ya kupooza ubongo kwani unaweza kumfanya mgonjwa akakamae mikono na miguu na hata kusababisha shingo yake ilegee.