Maelezo ya Chini
b Waisraeli hawakuwatangazia Wakanaani masharti ya amani kabla ya kupigana nao. Kwa nini? Kwa sababu Wakanaani walipewa miaka 400 ya kurekebisha matendo yao maovu. Kufikia wakati ambapo Waisraeli walipigana nao, Wakanaani walikuwa waovu sana. (Mwanzo 15:13-16) Hivyo, walipaswa kuangamizwa kabisa. Hata hivyo, Wakanaani waliobadilika waliokolewa.—Yoshua 6:25; 9:3-27.