Maelezo ya Chini
a Mkristo anaweza kuamua kumiliki bunduki kwa kusudi la kuwinda ili apate chakula au kujilinda dhidi ya wanyama wa mwituni. Hata hivyo, wakati ambapo silaha hizo hazitumiwi, inafaa zisiwe na risasi, au hata zitenganishwe sehemu-sehemu, na kufungiwa mahali salama. Katika nchi ambazo sheria haiwaruhusu watu kumiliki bunduki au bastola, au kuna vizuizi vya kumiliki silaha hizo, au serikali inadhibiti umiliki wake, Wakristo hutii sheria hizo.—Rom. 13:1.