Maelezo ya Chini
a Mwongozo kutoka Huduma ya Afya ya Kitaifa ya Uingereza unasema hivi: “Vitanzi vyenye shaba nyingi vinazuia mimba kwa zaidi ya asilimia 99. Hiyo inamaanisha kwamba ni wanawake wasiozidi asilimia moja wanaotumia vitanzi watakaopata mimba katika muda wa mwaka mmoja. Vitanzi vyenye shaba kidogo vina uwezo mdogo wa kuzuia mimba.”