Maelezo ya Chini
b UFAFANUZI WA MANENO: Mwanamume au mwanamke aliye mtu mzima anapomtumia mtoto kutosheleza tamaa zake za kingono anasemwa kwamba amemtendea vibaya kingono. Hilo linatia ndani kufanya ngono na mtoto; ngono ya kinywa au ya mkundu; kupapasa-papasa viungo vyake vya uzazi, matiti, au matako; au matendo mengine yaliyopotoka. Ni muhimu kutambua kwamba mtoto aliyetendewa vibaya kingono ameumizwa kihisia na kimwili na amedhulumiwa haki zake, na hapaswi kulaumiwa kwa jambo lililotendeka. Ingawa idadi kubwa ya wale wanaotendewa vibaya kingono ni wasichana, wavulana wengi pia hutendewa hivyo. Ingawa idadi kubwa ya watu wanaowatendea watoto vibaya kingono ni wanaume, baadhi ya wanawake pia hufanya hivyo.