Maelezo ya Chini
b UFAFANUZI WA MANENO: Katika makala hii na inayofuata, neno “uchumba” linarejelea kipindi ambacho mwanamume na mwanamke wanafahamiana vizuri zaidi ili kuamua ikiwa wanaweza kuwa wenzi wa ndoa. Katika nchi nyingine, neno hilo hurejelewa pia kuwa urafiki wa kimapenzi, kumjua vizuri zaidi mtu fulani, au uhusiano wa kimahaba. Uchumba unaanza wakati mwanamke na mwanamume wanapoelezana kwamba kila mmoja anavutiwa na mwenzake kimahaba, na unaendelea mpaka wanapoamua kufunga ndoa au kuvunja uchumba.