Maelezo ya Chini
a Vitabu vya Injili na vitabu vingine vya Biblia vina rekodi ya pindi nyingi ambazo Yesu aliyefufuliwa aliwatokea watu wengine, kama vile Maria Magdalene (Yoh. 20:11-18); wale wanawake wengine (Mt. 28:8-10; Luka 24:8-11); wale wanafunzi wawili (Luka 24:13-15); Petro (Luka 24:34); mitume isipokuwa Tomasi (Yoh. 20:19-24); mitume, pamoja na Tomasi (Yoh. 20:26); wanafunzi 7 (Yoh. 21:1, 2); zaidi ya wanafunzi 500 (Mt. 28:16; 1 Kor. 15:6); Yakobo, ndugu yake (1 Kor. 15:7); mitume wote (Mdo. 1:4); na mitume karibu na Bethania. (Luka 24:50-52) Huenda pindi nyingine ambazo Yesu aliwatokea watu hazikurekodiwa.—Yoh. 21:25.