Maelezo ya Chini
d Wasamoa huwa na jina moja, kama vile Pele, halafu jina la familia. Jina la familia la Pele ni Fuaiupolu. Pia, kuna Wasamoa ambao hupewa jina linalowakilisha ukoo mzima. Baadhi ya Mashahidi wa Yehova huyakataa majina hayo, kwa kuwa wanayaona kuwa ya kisiasa au ya kilimwengu. Kwa sababu hiyo, katika masimulizi haya tutatumia jina la kwanza na jina la familia linalojulikana sana, kama vile Pele Fuaiupolu.