Maelezo ya Chini
a Zamani nchi ya Myanmar iliitwa Burma, jina linalotokana na kabila kubwa zaidi la Myanmar linaloitwa Bamar (Waburma). Mnamo 1989 nchi hiyo ilipewa jina jipya, Muungano wa Myanmar, ili kuwakilisha makabila mengine mengi yaliyo nchini humo. Tutatumia jina Burma katika matukio yaliyotokea kabla ya mwaka 1989 na jina Myanmar katika matukio yaliyotokea baada mwaka huo.