Maelezo ya Chini
d Kalenda ya kisasa ya Kiyahudi inatumia makadirio ya wataalamu wa elimu ya nyota kuamua mwezi wa Nisani unaanza lini, lakini njia hiyo haikutumiwa katika karne ya kwanza. Badala yake, mwezi wa Nisani ulianza wakati ambapo mwezi mpya ulionekana kwa mara ya kwanza Yerusalemu, na hilo linaweza kuwa siku moja au zaidi baada ya makadirio yaliyo kwenye kalenda ya kisasa ya Kiyahudi. Hiyo ni sababu moja inayofanya tarehe ambayo Mashahidi wa Yehova huadhimisha Mlo wa Jioni wa Bwana kuwa tofauti na tarehe ambayo Wayahudi huadhimisha Pasaka leo.