Maelezo ya Chini
a Yonathani anapotajwa kwa mara ya kwanza katika simulizi la Biblia, mwanzoni mwa utawala wa Sauli, alikuwa kamanda wa jeshi, hivyo, lazima awe alikuwa na umri wa zaidi ya miaka 20. (Hesabu 1:3; 1 Samweli 13:2) Sauli alitawala kwa miaka 40. Kwa hiyo, kufikia wakati ambapo Sauli anakufa, Yonathani alikuwa na umri wa miaka 60 hivi. Daudi alikuwa na umri wa miaka 30 Sauli alipokufa. (1 Samweli 31:2; 2 Samweli 5:4) Kwa hiyo, ni wazi kwamba Yonathani alimzidi Daudi umri kwa miaka 30.