Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Matibabu Mengine Bora Badala ya Damu
    Damu Yaweza Kuokoaje Uhai Wako?
    • kuepuka utiaji-damu mishipani. Sisi tunatumaini kwamba wewe hutapoteza kamwe kiasi kikubwa cha damu. Lakini ukipoteza, inaelekea sana kwamba madaktari stadi wangeweza kukutunza bila kutumia utiaji-damu mishipani, ambao una hatari nyingi sana.

      UPASUAJI, NDIYO—LAKINI BILA UTIAJI-DAMU MISHIPANI

      Leo watu wengi hawatapokea damu. Kwa sababu za kiafya, wao wanaomba jambo ambalo Mashahidi hutafuta sana-sana kwa msingi wa kidini: utibabu bora kwa kutumia njia nyingine zisizotumia damu. Kama tulivyoona, upasuaji mkubwa ungali unawezekana. Kama una tashwishi zinazokawia-kawia, uthibitisho mwingine kutoka fasihi za kitiba huenda ukazifukuzia mbali.

      Ile makala “Kuwekwa kwa Viungo Vinne Vikubwa Badala ya Vilivyoharibika Katika Mshiriki wa Mashahidi wa Yehova” (Orthopaedic Review, Agosti 1986) ilisimulia juu ya mgonjwa mwenye kupungukiwa damu aliyekuwa na “uharibifu ulioendelea sana wa magoti na nyonga zote mbili.” Dextran ya chuma ilitumiwa kabla na baada ya upasuaji uliofanywa, ambao ulifanikiwa. Jarida British Journal of Anaesthesia (1982) liliripoti juu ya Shahidi mwenye umri wa miaka 52 aliyekuwa na kiwango cha hemoglobini kilichokuwa chini ya 10. Kwa kutumia njia ya hypotensive anesthesia (upotezaji fahamu kwa kutumia nusukaputi ili kushusha sana kanieneo ya damu) kupunguza upotezaji damu, nyonga na bega lake vilibadilishwa kabisa na kuwekwa vingine. Kikundi cha upasuaji kwenye Chuo Kikuu cha Arkansas (U.S.A.) kilitumia pia njia ii hii kubadilisha nyonga mia moja na kuweka nyingine kwa Mashahidi na wagonjwa wote wakapona. Profesa aliyekuwa akiongoza idara hiyo atoa elezo hili: “Jambo ambalo tumejifunza kutoka kwa wagonjwa hao (Mashahidi), tunatumia sasa kwa wagonjwa wetu wote ambao [tunabadilisha] nyonga kabisa.”

      Dhamiri za baadhi ya Mashahidi huwaruhusu wapokee mapandikizo ya viungo yakifanywa bila damu. Ripoti moja juu ya mapandikizo 13 ya figo ilifikia mkataa huu: “Matokeo ya ujumla huonyesha kwamba upandikizaji wa mafigo unaweza kutumiwa kwa Mashahidi wa Yehova kwa usalama na kwa mafanikio.” (Transplantation, Juni 1988) Vivyo hivyo, kukataa damu hakukuzuia hata mapandikizo ya moyo yenye mafanikio.

      Huenda ukauliza, ‘Namna gani upasuaji wa namna nyingine usiotumia damu?’ Jarida Medical Hotline (Aprili/Mei 1983) lilisimulia juu ya “Mashahidi wa Yehova waliopata mipasuo mikubwa ya viungo vya uzazi vya wanawake na iliyohusu mimba na kuzaa [kwenye Chuo Kikuu cha Mkoa wa Wayne, U.S.A.] bila utiaji-damu mishipani.” Karatasi-habari iliripoti hivi: “Hakukuwa na vifo na matatanisho zaidi kuliko ilivyokuwa katika wanawake waliokuwa wamepata upasuaji unaofanana na huo pamoja na utiwaji-damu mishipani.” Ndipo karatasi-habari ikatoa maelezo haya: “Matokeo ya uchunguzi huu huenda yakatoa sababu ya kuchunguza upya utumizi wa damu kwa wanawake wote wanaopata mipasuo ya viungo vya uzazi na inayohusu mimba na kuzaa.”

      Kwenye hospitali ya Chuo Kikuu cha Göttingen (Ujeremani), wagonjwa 30 waliokataa damu walipata upasuaji wanaofanyiwa watu wengi. “Hakuna matatanisho yaliyotokea ambayo hayangaliweza kutokea pia kwa wagonjwa wanaopokea utiwaji-damu mishipani. . . . Kwamba kutumia utiaji-damu mishipani hakuwezekani hakupasi kukadiriwa kupita kiasi, na hivyo hakupasi kuongoza kwenye kuacha kufanya upasuaji unaohitajiwa kabisa na ulio haki kufanywa kwa njia ya kupasua.”—Risiko in der Chirurgie, 1987.

      Hata upasuaji wa ubongo bila kutumia damu umefanywa juu ya watu wazima na watoto wengi, mathalani, kwenye Kitovu cha Kitiba cha Chuo Kikuu cha New York. Katika 1989 Dakt. Joseph Ransohoff, kiongozi wa upasuaji wa neva, aliandika: “Ni wazi sana kwamba katika visa vilivyo vingi ujiepushaji na vitu vilivyofanyizwa kwa damu waweza kufikiwa kukiwa na hatari kidogo sana kwa wagonjwa walio na itikadi za kidini dhidi ya utumizi wa vifanyizo hivyo, hasa ikiwa upasuaji utafanywa mara hiyo na kwa muda mfupi wa kupasua kwa uhusianifu. Wenye kupendeza sana ni uhakika wa kwamba mimi mara nyingi husahau kwamba mgonjwa ni Shahidi mpaka wakati wa kumwachilia wanaponishukuru kwa kuwa nilistahi imani zao.”

      Hatimaye, je! upasuaji mgumu unaohusu moyo na mishipa waweza kufanywa juu ya watu wazima na watoto bila damu? Dakt. Denton A. Cooley alikuwa mtangulizi katika kufanya jambo ilo hilo. Kama unavyoweza kuona katika makala ya kitiba iliyochapwa upya katika Nyongeza, katika kurasa 27-9, ukitegemea uchanganuzi wa mapema zaidi, mkataa wa Dakt. Cooley ulikuwa “kwamba hatari ya upasuaji katika kikundi cha wagonjwa Mashahidi wa Yehova haikuwa juu sana kuliko ya [vikundi] vingine.” Sasa, baada ya kufanya 1,106 ya mipasuo hii, yeye aandika: “Katika kila kisa mwafaka au mkataba wangu na mgonjwa hudumishwa,” yaani, kutotumia damu.

      Madaktari wapasuaji wameona kwamba mtazamo mzuri ni jambo jingine walilo nalo Mashahidi wa Yehova. “Mtazamo wa wagonjwa hawa umekuwa kielelezo kizuri,” akaandika Dakt. Cooley katika Oktoba 1989. “Wao hawana hofu waliyo nayo wagonjwa walio wengi ya matatanisho au hata ya kifo. Wana imani yenye kina na yenye kudumu katika itikadi yao na katika Mungu wao.”

      Hii haimaanishi kwamba wao husisitizia haki ya kufa. Wao hufuatia kwa bidii utunzaji bora kwa sababu wanataka kupona. Wamesadikishwa kwamba kutii sheria ya Mungu juu ya damu ni jambo la hekima, jambo ambalo linakuwa na uvutano chanya katika upasuaji usiotumia damu.

      Profesa Dakt. V. Schlosser, wa hospitali ya upasuaji kwenye Chuo Kikuu cha Freiburg (Ujeremani), aliandika: “Miongoni mwa wagonjwa wa kikundi hiki, tukio la kutokwa damu wakati wa pindi ya upasuaji halikuwa la juu zaidi; kwa vyovyote, matatanisho yalikuwa machache zaidi. Yale maoni ya pekee juu ya ugonjwa, waliyo nayo Mashahidi wa Yehova, yalikuwa na uvutano chanya wakati wa pindi ya upasuaji.”—Herz Kreislauf, Agosti 1987.

  • Wewe Una Haki ya Kuchagua
    Damu Yaweza Kuokoaje Uhai Wako?
    • Wewe Una Haki ya Kuchagua

      Njia ya kisasa ya kitiba (iitwayo uchanganuzi wa hatari/manufaa) inafanya iwe rahisi zaidi kwa madaktari na wagonjwa kushirikiana katika kuepuka utibabu wa kutumia damu. Madaktari hupima mambo kama vile hatari za madawa au upasuaji na manufaa zinazoweza kuwapo. Wagonjwa waweza pia kushiriki katika uchanganuzi huo.

      Acheni tutumie kielelezo kimoja ambacho watu wengi wanaweza kujihusisha nacho—ugonjwa wenye kusedeka wa tezi za kooni. Kama ungekuwa na tatizo hilo inaelekea ungeenda kwa daktari. Kwa kweli, huenda ukawaona wawili, kwa kuwa mara nyingi wataalamu wa afya hupendekeza kupata wazo la pili. Huenda mmoja akapendekeza upasuaji. Atoa muhtasari wa kinachomaanishwa na hilo: Muda wa kukaa hospitalini, kiasi cha

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki