Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w94 10/1 uku. 31
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
  • Habari Zinazolingana
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
  • Kubali Mwongozo wa Mungu Aliye Hai
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
w94 10/1 uku. 31

Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Je, ingekuwa sawa kukubali dawa ya chanjo au ya sindano nyingine yoyote ya kitiba yenye albumini itokayo katika damu ya binadamu?

Kusema wazi, ni lazima kila Mkristo aamue binafsi suala hili.

Kwa kufaa watumishi wa Mungu wataka kutii mwongozo upatikanao kwenye Matendo 15:28, 29, wa kuepuka damu. Kwa hiyo, Wakristo hawawezi kula nyama isiyoondolewa damu au vyakula kama soseji za damu. Lakini sheria ya Mungu yatumika pia kwa hali ya kitiba. Mashahidi wa Yehova hubeba hati isemayo kwamba wao wakataa ‘mitio ya damu mishipani, damu nzima, chembe nyekundu, chembe nyeupe, visahani, au plazima ya damu.’ Lakini vipi juu ya kudungwa dawa za seramu zenye vipimo kidogo sana za protini za damu?

Kwa muda mrefu Mashahidi wametambua kwamba hili ni suala la uamuzi wa binafsi kwa kupatana na dhamiri ya kila mtu iliyozoezwa na Biblia. Jambo hilo lilitajwa katika makala “Maswali Kutoka kwa Wasomaji” ya Mnara wa Mlinzi la Juni 1, 1990, iliyozungumzia dawa za kudungwa za seramu ambazo tabibu aweza kupendekeza iwapo kuna hatari ya kushikwa na maradhi fulani. Sehemu kuu zifanyazo kazi za dawa hizo za kudungwa si plazima ya damu pekee bali ni viuajisumu vitolewavyo kutoka kwa plazima ya damu ya wanadamu au wanyama ambao wamesitawisha kinga kwa maradhi hayo. Baadhi ya Wakristo wanaohisi kwamba wao waweza kwa dhamiri njema kukubali dawa za kudungwa kama hizo wameona kwamba viuajisumu kutoka kwa damu ya mwanamke mja-mzito huingia katika damu ya mtoto aliye katika tumbo lake la uzazi. “Maswali Kutoka kwa Wasomaji” ilitaja jambo hili, na vilevile kwamba kiasi fulani cha albumini hupita kutoka kwa mwanamke mja-mzito na kuingia kwa mtoto wake.

Watu wengi huona hilo kuwa jambo la kufikiriwa, kwa kuwa baadhi ya dawa fulani za chanjo ambazo hazifanyizwi kwa damu zaweza kubeba kiasi kidogo sana cha albumini ya plazima iliyotumiwa au kuongezwa ili kusawazisha viungo vya dawa hizo katika matayarisho. Kwa sasa kiasi kidogo cha albumini pia chatumiwa katika dawa za kudungwa za hormoni iliyotengenezwa iitwayo EPO (erythropoietin). Mashahidi fulani wamekubali dawa za kudungwa za EPO kwa sababu hiyo yaweza kuharakisha ufanyizwaji wa chembe nyekundu za damu na hivyo yaweza kuondolea tabibu hisia ya kwamba mitio ya damu mishipani yaweza kuhitajiwa.

Huenda dawa nyinginezo za kitiba zenye kiwango kidogo zaidi ya albumini zikafanyizwa zitumiwe katika wakati ujao, kwa kuwa kampuni za kutengeneza dawa hufanyiza dawa mpya au kubadili mifanyizo ya dawa zilizopo. Kwa hiyo huenda Wakristo wakataka kufikiria kama albumini ni sehemu kuu ya dawa ya chanjo au dawa ya kudungwa ambayo daktari apendekeza. Kama wana shaka au wana sababu za kuamini kwamba albumini inafanyiza sehemu kuu ya dawa hiyo, wao waweza kuuliza tabibu wao.

Kama ilivyotaja, Mashahidi wengi hawajakataa dawa ya kudungwa yenye kiasi kidogo cha albumini. Na bado, mtu yeyote atakaye kujifunza habari hii kikamili zaidi kabla ya kuamua binafsi apaswa kupitia habari iliyomo katika “Maswali Kutoka kwa Wasomaji” la Mnara wa Mlinzi la Juni 1, 1990.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki