Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kusalimu Bendera, Kupiga Kura, na Utumishi wa Kiraia
    “Jitunzeni Katika Upendo wa Mungu”
    • Dhamiri ya Mkristo fulani ikimruhusu kufanya utumishi fulani wa kiraia ili aepuke kufungwa gerezani, Wakristo wenzake wanapaswa kuheshimu uamuzi wake. (Waroma 14:10) Lakini ikiwa anaona kwamba hawezi kufanya utumishi huo, wengine wanapaswa kuheshimu uamuzi huo pia.—1 Wakorintho 10:29; 2 Wakorintho 1:24.

  • Visehemu vya Damu na Mbinu Zinazotumiwa na Madaktari
    “Jitunzeni Katika Upendo wa Mungu”
    • NYONGEZA

      Visehemu vya Damu na Mbinu Zinazotumiwa na Madaktari

      Visehemu vya damu. Visehemu vya damu hutokana na zile sehemu nne kuu za damu, yaani, chembe nyekundu, chembe nyeupe, chembelele (platelets), na utegili (plasma). Kwa mfano, chembe nyekundu zina protini inayoitwa himoglobini. Dawa ambazo zinatengenezwa kutokana na himoglobini ya binadamu au mnyama hutumiwa kutibu wagonjwa wenye upungufu wa damu au waliopoteza damu nyingi.

      Utegili—ambao asilimia 90 yake ni maji—una homoni mbalimbali, chumvi, vimeng’enya, na lishe, kutia ndani madini na sukari. Pia, utegili huwa na vigandisha-damu, kingamwili zinazopigana na magonjwa, na protini kama vile albumini. Mtu akipata ugonjwa fulani, madaktari wanaweza kupendekeza adungwe sindano yenye kingamwili (gamma globulin), ambayo inatengenezwa kutokana na utegili wa watu ambao tayari wana kinga ya ugonjwa huo. Protini fulani (interferons na interleukins) zinaweza kutolewa katika chembe nyeupe za damu na kutumiwa kutibu magonjwa fulani ya virusi na kansa mbalimbali.

      Je, Wakristo wanaweza kukubali matibabu yanayohusisha visehemu vya damu? Biblia haitoi maagizo ya moja kwa moja, kwa hiyo kila mtu anapaswa kujiamulia kulingana na dhamiri yake mwenyewe mbele za Mungu. Huenda wengine wakakataa visehemu vyote, wakisema kwamba kulingana na Sheria ambayo Mungu aliwapa Waisraeli, damu ambayo ilitolewa kwa kiumbe ilipaswa ‘kumwagwa kwenye udongo.’ (Kumbukumbu la Torati 12:22-24) Ingawa wengine wanakataa kutiwa damu mishipani

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki