Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kutangaza Mnara wa Mlinzi
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Kutafsiriwa kwa Watch Tower katika lugha nyinginezo kulianza polepole. Toleo moja la kielelezo lilichapwa katika Kisweden katika 1883 ili litumiwe kuwa trakti. Kuanzia 1886 hadi 1889, chapa ndogo ya gazeti hili ilichapwa katika Kijerumani. Lakini haikuwa hadi 1897 kwamba Watch Tower lilitokea tena katika Kijerumani na likaendelea kutangazwa bila kukoma. Kufikia 1916 lilikuwa likichapwa katika lugha saba—Kidenmark-Kinorway, Kifaransa, Kifinland, Kiingereza, Kijerumani, Kipoland, na Kisweden. Wakati kuhubiriwa kwa habari njema kulipoongeza mwendo zaidi katika 1922, hesabu ya lugha ambazo gazeti hilo lilitangazwa iliongezwa kuwa 16. Hata hivyo, kufikia 1993, lilikuwa likitokezwa kwa ukawaida katika lugha 112—zile zinazotumiwa na sehemu kubwa ya idadi ya watu duniani. Hiyo ilitia ndani si lugha kama vile Kiingereza, Kihispania, na Kijapani tu, ambazo kwazo mamilioni ya nakala za kila toleo zilichapwa, bali pia Kipalau, Kituvalu, na nyinginezo ambazo ni mia chache zilizokuwa zikigawanywa.

      Kwa miaka mingi Mnara wa Mlinzi lilionwa kuwa gazeti hasa la “kundi dogo” la Wakristo waliojitakasa. Hesabu ya nakala zilizotokezwa ilikuwa ndogo; kufikia 1916 ni nakala 45,000 tu zilizokuwa zikichapwa. Lakini kuanzia 1935, mkazo wa mara kwa mara uliwekwa juu ya kuwatia moyo “Wayonadabu,” au “umati mkubwa,” wapate na kusoma Mnara wa Mlinzi kwa ukawaida. Katika 1939, wakati jalada la gazeti hilo lilipoanza kukazia Ufalme, maandikisho ya Mnara wa Mlinzi yalitolewa kwa umma wakati wa kampeni ya uandikishaji ya kimataifa ya miezi minne. Kama tokeo, orodha ya maandikisho ilipanda ikawa 120,000. Mwaka uliofuata, Mnara wa Mlinzi lilikuwa likitolewa kwa watu barabarani kwa ukawaida. Hesabu ya nakala zilizotokezwa iliongezeka upesi. Kufikia mapema 1993 uchapaji wa kila toleo ulikuwa 16,400,000.

  • Amkeni!—Gazeti Linalovutia Sana Umma
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Kuanzia toleo la Oktoba 6, 1937, kichwa kilibadilishwa kuwa Consolation. Hicho kilifaa sana kwa sababu ya uonevu ambao wengi walikuwa wakipata na msukosuko ambao ulimwengu ulijitia ndani yao katika Vita ya Ulimwengu 2. Hata hivyo, kitulizo ambacho gazeti hilo lilitoa, kilikuwa cha aina ile inayovutia wale tu walio na upendo halisi wa ile kweli.

      Kuanzia toleo la Agosti 22, 1946, kichwa Amkeni! kilianza kutumiwa. Mkazo uliwekwa juu ya kuwaamsha watu waone umaana wa matukio ya ulimwengu. Gazeti hili lilitumia vyanzo vya habari vilivyo mashuhuri, lakini pia lilikuwa na waleta habari walo lenyewe duniani pote. Makala za Amkeni! zilizo na usawaziko, zinazotumika na za kina kirefu ambazo huzungumzia habari nyingi mbalimbali hutia moyo wasomaji wafikiri juu ya ujumbe wa maana zaidi wa gazeti hili, yaani, kwamba matukio ya ulimwengu hutimiza unabii wa Biblia, unaoonyesha kwamba tunaishi katika siku za mwisho na kwamba karibuni Ufalme wa Mungu utaleta manufaa za milele kwa wale wanaojifunza na kufanya mapenzi ya Mungu. Gazeti hili limekuwa chombo chenye matokeo katika kupiga mbiu juu ya habari njema za Ufalme wa Mungu duniani pote na limekuwa daraja kwa funzo la habari ya kina kirefu inayopatikana katika Mnara wa Mlinzi na vitabu vilivyojalidiwa.

      Kufikia mapema 1993, Amkeni! lilikuwa likichapwa katika lugha 67, nakala 13,240,000 kwa kila toleo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki