-
Mungu Si wa Polepole kwa Habari ya Ahadi YakeMnara wa Mlinzi—1999 | Juni 1
-
-
Kiwango cha Uovu Kukamilika
Tunapochunguza jinsi Mungu alivyoshughulika na wanadamu wakati uliopita, tunaona kwamba mara nyingi alizuia hukumu yake hadi wakati ambapo hakukuwa na tumaini lolote la hali kubadilika. Kwa mfano, kuhusiana na hukumu yake dhidi ya Wakanaani, Mungu alimtajia Abrahamu dhambi zao mapema sana. Lakini wakati wa kutekelezwa kwa hukumu yake haukuwa umefika. Kwa nini? Biblia husema: “Maana haujatimia uovu wa Waamori [Wakanaani] bado,” au kama tafsiri ya Knox isemavyo: “Uovu wa Waamori [haukuwa] umekamilika kabisa.”—Mwanzo 15:16.a
Hata hivyo, miaka ipatayo 400 baadaye, hukumu ya Mungu ilitekelezwa, nao Waisraeli, wazao wa Abrahamu, wakatwaa nchi hiyo. Wakanaani kadhaa waliokolewa, kama vile Rahabu, na Wagibeoni, kwa sababu ya mtazamo wao na matendo yao, lakini kwa ujumla, ukosefu wao wa usafi ulikuwa umefikia kiwango kikubwa mno, kama inavyofunuliwa na uchimbuzi wa kiakiolojia. Waliabudu mifano ya uume, wakafanya umalaya hekaluni, na kutoa watoto wakiwa dhabihu. Kichapo Halley’s Bible Handbook chasema hivi: “Waakiolojia ambao huchimbua kwenye magofu ya majiji ya Kanaani hujiuliza ni kwa nini Mungu hakuwaangamiza hata mapema zaidi ya wakati alipofanya hivyo.” Hatimaye, ‘kiwango cha dhambi za Wakanaani kikakamilika’; uovu wao ukawa ‘umekamilika kabisa.’ Hakuna yeyote ambaye kwa haki angeweza kumlaumu Mungu kuwa mwenye kukosa haki aliporuhusu nchi hiyo isafishwe huku akiwaokoa wale walioonyesha mtazamo unaofaa.
-
-
Mungu Si wa Polepole kwa Habari ya Ahadi YakeMnara wa Mlinzi—1999 | Juni 1
-
-
a Kielezi-chini cha mstari huo katika kichapo The Soncino Chumash chasema hivi: “Kustahili kufukuzwa, kwa kuwa Mungu haadhibu taifa hadi kiwango chake cha dhambi kikamilike.”
-