-
Kimbelembele Hutokeza AibuMnara wa Mlinzi—2000 | Agosti 1
-
-
7. (a) Musa alishughulikaje na Kora na wafuasi wake? (b) Maasi ya Kora yalimalizwaje kwa msiba?
7 Musa akawaambia Kora na watu wake wakusanyike kwenye hema la kukutania kesho yake asubuhi wakiwa na chetezo na uvumba. Kora na wafuasi wake hawakuruhusiwa kufukiza uvumba kwa sababu hawakuwa makuhani. Kama wangekuja na chetezo na uvumba, ingekuwa wazi kwamba watu hao bado waliona wana haki ya kuwa makuhani—hata baada ya kuwa na fursa ya kulifikiria jambo hilo usiku kucha.
-