-
Mwamuzi Anayehukumu kwa HakiMnara wa Mlinzi—2009 | Septemba 1
-
-
Musa alitii mambo mawili ya kwanza, lakini hakutii jambo la tatu. Badala ya kuzungumza na mwamba kwa imani, alizungumza na watu kwa uchungu akisema: “Sikieni, sasa, enyi waasi! Je, tuwatolee ninyi maji katika mwamba huu?” (Mstari wa 10; Zaburi 106:32, 33) Kisha Musa akaupiga mwamba mara mbili, “na maji mengi yakaanza kutoka.”—Mstari wa 11.
Kwa sababu hiyo, Musa, pamoja na Haruni, wakafanya dhambi nzito. “Ninyi mliasi agizo langu,” Mungu akawaambia. (Hesabu 20:24) Pindi hii walipotenda kinyume cha agizo la Mungu, Musa na Haruni wakawa kile walichowaita watu wale wengine, yaani, wakawa waasi.
-
-
Mwamuzi Anayehukumu kwa HakiMnara wa Mlinzi—2009 | Septemba 1
-
-
Kwa kusema “tuwatolee ninyi maji,” Musa alizungumza kana kwamba yeye na Haruni—si Mungu—ndio waliokuwa wakiwaandalia maji hayo kimuujiza.
-