-
“Upanga wa Yehova na wa Gideoni!”Mnara wa Mlinzi—2005 | Julai 15
-
-
Askari hao 300 Waisraeli wanasonga polepole hadi kwenye ukingo wa kambi ya maadui. Ni saa nne hivi za usiku, baada tu ya walinzi kubadilishana zamu. Huu waonekana kuwa wakati bora wa kushambulia, kwani itachukua muda fulani kwa walinzi ambao wametoka tu kuanza zamu yao kuona vizuri gizani.
-