-
“Mwanamke Bora Sana”Mnara wa Mlinzi—2012 | Oktoba 1
-
-
RUTHU alipiga magoti kando ya vishina vya shayiri ambavyo alikuwa amekusanya wakati wa mchana. Giza lilikuwa likiingia kwenye mashamba karibu na Bethlehemu, na wafanyakazi wengi tayari walikuwa wakielekea kwenye lango la jiji dogo ambalo lilikuwa juu ya bonde lililokuwa karibu. Ruthu alikuwa amechoka sana baada ya kufanya kazi mchana kutwa, yaani, tangu asubuhi. Lakini, aliendelea kupiga miganda akitumia ufito mdogo au gongo ili apate nafaka. Hata hivyo, ilikuwa siku njema, kuliko jinsi alivyotazamia.
-
-
“Mwanamke Bora Sana”Mnara wa Mlinzi—2012 | Oktoba 1
-
-
Ruthu alipomaliza kupura nafaka na kuikusanya, alitambua kwamba alikuwa amekusanya karibu kipimo kimoja cha efa, au lita 22 hivi za shayiri. Huenda mzigo wake ulikuwa na uzito wa kilo 14! Akauinua mzigo wake, labda akiwa ameufunga kwa kitambaa na kuubeba kichwani, kisha akatembea kuelekea Bethlehemu huku jua likitua.—Ruthu 2:17.
-