-
Barzilai—Mtu Aliyetambua Udhaifu WakeMnara wa Mlinzi—2007 | Julai 15
-
-
Ingawa bado alimuunga mkono Daudi, inaelekea kwamba Barzilai aliamini kwamba mwanamume kijana angeweza kutimiza migawo vizuri zaidi. Labda akizungumza kuhusu mwana wake mwenyewe, Barzilai alisema: “Tazama, mtumishi wako Kimhamu. Acha avuke pamoja na bwana wangu mfalme; nawe umfanyie yaliyo mema machoni pako.” Badala ya kuudhika, Daudi alikubali pendekezo hilo.
-