-
“Mwenyezi-Mungu . . . Amejaa Nguvu”Mkaribie Yehova
-
-
Kisa cha Eliya kilichotajwa mwanzoni ni mfano unaofaa. Kwa nini Yehova alimwonyesha tukio hilo la kustaajabisha la nguvu Zake? Malkia mwovu Yezebeli alikuwa ameapa kumwua Eliya. Nabii huyo alitoroka ili asiuawe. Alihisi upweke, aliogopa, na alikuwa amevunjika moyo—kana kwamba kazi yake yote ilikuwa ya bure. Yehova alimfariji Eliya aliyekuwa taabani kwa kumkumbusha waziwazi kuhusu nguvu Zake. Upepo, tetemeko la nchi, na moto vilionyesha kwamba Mungu mwenye nguvu zaidi katika ulimwengu wote alikuwa pamoja na Eliya. Kwa nini amhofu Yezebeli huku Yehova akiwa upande wake?—1 Wafalme 19:1-12.b
-
-
“Mwenyezi-Mungu . . . Amejaa Nguvu”Mkaribie Yehova
-
-
b Biblia inasema kwamba “BWANA hakuwamo katika upepo ule . . . , tetemeko la nchi . . . , moto ule.” Tofauti na wale wanaoabudu miungu ya kihekaya ya nguvu za asili, watumishi wa Yehova hawamtafuti katika nguvu za maumbile. Yeye ni mkuu sana hivi kwamba hawezi kuishi katika kitu chochote alichoumba.—1 Wafalme 8:27.
-