-
Aliwatetea Watu wa MunguMnara wa Mlinzi—2011 | Oktoba 1
-
-
Wazia jinsi tangazo hilo lilivyowaathiri mabaki ya Wayahudi waliokuwa mbali jijini Yerusalemu. Mabaki hao waliokuwa wamerudi kutoka uhamishoni Babiloni, walikuwa wakijitahidi kujenga upya jiji hilo ambalo halikuwa na kuta za kuwalinda. Huenda Mordekai aliposikia kuhusu habari hizo mbaya aliwafikiria Wayahudi hao waliokuwa Yerusalemu, rafiki zake, na watu wake wa ukoo waliokuwa Shushani. Akiwa amefadhaika alirarua mavazi yake, akavaa magunia, akajipaka majivu kwenye kichwa chake, na kulia kwa sauti ya juu katikati ya jiji.
-