-
Alitenda kwa Hekima, Ujasiri, na Bila UbinafsiMnara wa Mlinzi—2012 | Januari 1
-
-
Sasa kwa kuwa Esta na Mordekai walikuwa salama, je, malkia angetulia na kustarehe? Angefanya hivyo tu ikiwa angekuwa na ubinafsi. Wakati huo, agizo la Hamani la kuwaua Wayahudi wote bado lilikuwa likisambazwa kotekote katika milki hiyo. Hamani alikuwa amepiga kura, au Puri—labda njia fulani ya kuwasiliana na pepo—ili kuamua wakati uliofaa wa kutekeleza mashambulizi hayo ya kikatili. (Esta 9:24-26) Bado miezi kadhaa ilibaki kabla ya siku hiyo kufika, lakini muda ulikuwa unayoyoma. Je, msiba huo ungeepukwa?
Esta alitenda bila ubinafsi na akahatarisha uhai wake tena kwa kwenda mbele ya mfalme bila kuitwa. Wakati huu, alilia kwa ajili ya watu wake, na kumsihi mume wake afutilie mbali agizo baya alilokuwa ametoa.
-