Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Tazameni Mtekelezaji wa Mambo ya Ajabu!
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Aprili 15
    • Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani? Au ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni?”—Ayubu 38:4-6.

  • Tazameni Mtekelezaji wa Mambo ya Ajabu!
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Aprili 15
    • Akiifananisha dunia yetu na jengo, Mungu aliuliza hivi: “Ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni?” Tunajua kwamba dunia imewekwa umbali hususa kutoka kwa jua, umbali unaotuwezesha kuishi na kufurahia maisha. Nayo dunia ina ukubwa ufaao. Kama dunia yetu ingalikuwa kubwa zaidi ya vile ilivyo sasa, gesi ya hidrojeni haingeweza kutoka katika angahewa letu nayo dunia haingekalika. Ni wazi kwamba mtu fulani ‘aliliweka jiwe lake la pembeni’ mahali pafaapo. Je, Ayubu alistahili sifa kwa jambo hilo? Je, sisi twastahili sifa? Au Yehova Mungu ndiye anayestahili sifa?—Mithali 3:19; Yeremia 10:12.

      Ni Mwanadamu Gani Awezaye Kutoa Majibu?

      12. Swali linalopatikana kwenye Ayubu 38:6 lafanya tufikirie nini?

      12 Mungu aliuliza hivi pia: “Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani?” Je, hilo si swali zuri? Huenda twajua nguvu za uvutano, jambo ambalo Ayubu hakujua. Wengi wetu twafahamu kwamba nguvu za uvutano za jua huwezesha dunia idumu mahali ilipo, kana kwamba misingi yake imekazwa. Hata hivyo, je, kuna yeyote kati yetu awezaye kuzielewa kikamili nguvu za uvutano?

      13, 14. (a) Ni lazima tukiri nini kuhusu nguvu za uvutano? (b) Tuoneje hali inayokaziwa na andiko la Ayubu 38:6?

      13 Kitabu kilichochapishwa hivi majuzi, The Universe Explained, chakiri kwamba ‘watu wengi wanazijua nguvu za uvutano, lakini hawazielewi vizuri kama wanavyoelewa nguvu nyinginezo za asili.’ Kitabu hicho chaendelea kusema: “Yaonekana kwamba nguvu za uvutano husafiri kasi angani, bila kufuata njia yoyote mahususi. Hata hivyo, katika miaka ya majuzi, wanafizikia wameanza kukisia kwamba huenda ikawa nguvu za uvutano husafiri kwa mawimbi ya chembe ndogo ziitwazo graviton . . . Lakini hakuna yeyote aliye na uhakika kwamba chembe hizo zipo.” Hebu wazia hilo lamaanisha nini.

      14 Sayansi imepiga hatua kubwa kwa miaka 3,000 tangu Yehova alipomwuliza Ayubu maswali hayo. Hata hivyo, wala sisi wala wataalamu wa fizikia hawawezi kueleza kikamili jinsi nguvu za uvutano zidumishavyo dunia katika mzunguko wake, mahali hasa ipaswapo kuwa ili kutuwezesha kufurahia maisha. (Ayubu 26:7; Isaya 45:18) Kusema hivyo hakudokezi kwamba sote tunahitaji kuanza uchunguzi wenye kina juu ya mambo tusiyoelewa kuhusu nguvu za uvutano. Hata hivyo, kuzingatia hata sehemu hii moja tu ya kazi za Mungu za ajabu kwapasa kuathiri maoni yetu kumhusu. Je, unastaajabia hekima yake na ujuzi wake, na je, unaelewa ni kwa nini twahitaji kujifunza mengi zaidi juu ya mapenzi yake?

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki