Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Zingatia Kazi za Mungu za Ajabu
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Aprili 15
    • 3. Mungu aliuliza juu ya mambo gani kwenye Ayubu 38:22-23, 25-29?

      3 Wakati mmoja, Mungu alimwuliza Ayubu hivi: “Je! umeziingia ghala za theluji, au umeziona ghala za mvua ya mawe, nilizoziweka akiba kwa wakati wa misiba, kwa siku ya mapigano na vita?” Theluji na mvua ya mawe hutokea katika sehemu nyingi za dunia yetu.

  • Zingatia Kazi za Mungu za Ajabu
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Aprili 15
    • Ayubu 38:22, 23,

  • Zingatia Kazi za Mungu za Ajabu
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Aprili 15
    • 4-6. Ni katika maana gani mwanadamu amekosa ujuzi kamili kuhusu theluji?

      4 Huenda watu fulani wanaoishi katika jamii zenye hekaheka nyingi, ambao ni lazima wasafiri, wakaiona theluji kuwa kizuizi. Hata hivyo, watu wengine huvutiwa sana na theluji wakati wa majira ya baridi kali kwa kuwa hiyo huwapa fursa ya kufanya mambo ya pekee. Unapofikiria swali ambalo Mungu aliuliza, je, wewe unaijua theluji vizuri, na je, umewahi kuiona? Tunajua jinsi rundo kubwa la theluji lilivyo, aidha kwa kuwa tumeliona kwa macho yetu wenyewe au tumeona picha zake. Lakini namna gani chembe za theluji? Je, wajua chembe za theluji zinafananaje, labda kwa kuchunguza jinsi zinavyotokea?

      5 Watu fulani wamechunguza na kupiga picha chembe za theluji kwa makumi ya miaka. Chembe moja ya theluji inaweza kuwa na chembe ndogondogo mia moja za barafu zenye maumbo mbalimbali yenye kupendeza. Kitabu kiitwacho Atmosphere chasema: ‘Namna nyingi za chembe za theluji zajulikana sana, na ingawa wanasayansi wanasisitiza kwamba hakuna sheria ya asili ambayo huzuia chembe hizo zisifanane, hawajawahi kupata chembe mbili zinazofanana. Wilson A. Bentley alifanya uchunguzi mkubwa uliochukua muda wa miaka 40 kwa kutumia darubini kupiga picha chembe za theluji, lakini hakupata chembe mbili zinazofanana.’ Na hata kama angalipata chembe mbili zinazofanana, jambo ambalo ni nadra, je, hilo lingebadili kwa njia yoyote maajabu tunayoona katika namna nyingi za chembe za barafu?

      6 Kumbuka swali la Mungu: “Je! umeziingia ghala za theluji?” Wengi hufikiria mawingu kuwa ghala za theluji. Je, waweza kuwazia ukiingia katika ghala hizo kuhesabu chembe za theluji za namna nyingi sana na kuchunguza jinsi zilivyotokea? Ensaiklopidia moja ya sayansi yasema hivi: ‘Asili ya kiini cha barafu, ambacho husababisha matone ya maji kwenye mawingu yagande wakati wa baridi kali, haijulikani bado.’—Zaburi 147:16, 17; Isaya 55:9, 10.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki