-
Ni Nani Anayeweza Kuwakomboa Wale Wanaolilia Msaada?Mnara wa Mlinzi—2010 | Agosti 15
-
-
20 Ni nani atakayesifiwa kwa ajili ya baraka hizo zote? Kwanza kabisa ni Mfalme wa Milele na Mtawala wa Ulimwengu Wote, Yehova Mungu. Kwa kweli, wakati huo sote tutaimba pamoja kwa shangwe sehemu ya mwisho ya wimbo huu mtamu unaochangamsha moyo: “Jina lake [la Mfalme Yesu Kristo] na liweko mpaka wakati usio na kipimo; jina lake na liongezeke mbele ya jua, na kupitia yeye na wajibariki; mataifa yote na yamtangaze kuwa mwenye furaha.
-