-
Furahia Kujifunza Kibinafsi Neno la MunguMnara wa Mlinzi—2002 | Desemba 1
-
-
9 Aendelea kusema: “Ukiutafuta [ufahamu] kama fedha, na kuutafutia kama hazina iliyositirika; . . .” (Mithali 2:4) Hilo lafanya tufikirie mafanikio ambayo wachimba-migodi wamepata kwa karne nyingi wakitafuta madini yanayoitwa eti yenye thamani kama vile fedha na dhahabu. Watu wamewaua wengine kwa sababu ya dhahabu. Wengine wametumia maisha yao yote wakitafuta dhahabu. Hata hivyo, dhahabu ina thamani gani? Ikiwa ungepotea jangwani na una kiu kali sana, ungechagua nini: kipande cha dhahabu au kikombe cha maji? Hata hivyo, watu wametafuta dhahabu kwa bidii licha ya kwamba thamani yake ni ya kijuujuu tu na hubadilika-badilika!a Tunapaswa kujitahidi sana kutafuta hekima, ufahamu, na uelewevu wa mapenzi ya Mungu! Lakini tutapata manufaa gani kwa kutafuta mambo hayo?—Zaburi 19:7-10; Mithali 3:13-18.
-
-
Furahia Kujifunza Kibinafsi Neno la MunguMnara wa Mlinzi—2002 | Desemba 1
-
-
a Tangu mwaka wa 1979 thamani ya dhahabu imeshuka kutoka dola za Marekani 850.00 kwa gramu 31 mwaka wa 1980 hadi dola za Marekani 252.80 kwa gramu 31 mwaka wa 1999.
-