-
Pata Hekima na Ukubali NidhamuMnara wa Mlinzi—1999 | Septemba 15
-
-
Kufahamu mithali na kitendawili, na maneno ya wenye hekima na mafumbo yao.” (Mithali 1:5, 6, italiki ni zetu.)
-
-
Pata Hekima na Ukubali NidhamuMnara wa Mlinzi—1999 | Septemba 15
-
-
Mara nyingi mithali hutoa maana yenye kutokeza katika maneno machache sana. Huenda mithali ya Biblia ikawa msemo wenye kutatanisha. (Mithali 1:17-19) Mithali nyingine ni mafumbo—taarifa zenye kutatanisha na ngumu zinazohitaji kufumbuliwa. Huenda mithali pia ikatia ndani tashbihi, sitiari, na tamathali nyingine za usemi. Inahitaji muda na kutafakari ili kuzielewa. Bila shaka, Solomoni, aliyetunga mithali nyingi sana, alikuwa na uwezo wa kuzielewa. Katika kitabu cha Mithali, anajitwika daraka la kuwapa wasomaji wake uwezo huo, jambo ambalo mtu mwenye hekima angetaka kuzingatia.
-