-
Unaweza Kudumisha Usafi wa Kiadili Katika Ulimwengu Usio na MaadiliMnara wa Mlinzi—2000 | Julai 15
-
-
Jihadhari na Kinywa Laini
Linalofanya uwezo wa kufikiri uwe wa maana katika kudumisha usafi wa kiadili katika ulimwengu mchafu ni kwa sababu njia za mtu asiye mwadilifu huvutia. Solomoni aonya hivi: “Maana midomo ya malaya [“mwanamke mgeni,” “NW”] hudondoza asali, na kinywa chake ni laini kuliko mafuta;
-
-
Unaweza Kudumisha Usafi wa Kiadili Katika Ulimwengu Usio na MaadiliMnara wa Mlinzi—2000 | Julai 15
-
-
Katika mithali hii, mtu mpotovu aitwa “mwanamke mgeni”—malaya.a Maneno yake ya kutongoza ni matamu kama asali na ni laini kuliko mafuta ya zeituni. Je, mara nyingi kutongoza hakuanzi hivyo? Kwa mfano, fikiria yaliyompata mwanamke mrembo wa miaka 27 aitwaye Amy, ambaye ni karani. Yeye anasimulia: “Kuna mwanamume fulani kazini kwetu ambaye huniangalia daima na kunisifu kila wakati. Inapendeza kuonyeshwa shauku. Lakini naweza kuona waziwazi kuwa anataka tu kulala nami. Mimi sitadanganywa na utongozaji wake.” Kwa kawaida maneno laini ya mtongozaji hunasa haraka tukishindwa kutambua lengo lake. Kwa sababu hiyo tunahitaji kutumia uwezo wetu wa kufikiri.
-