Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Unatimiza Wajibu Wako Wote kwa Mungu?
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Novemba 15
    • Yeye alisema: “Maneno yao wenye hekima huwa mfano wa michokoro; na kama misumari iliyogongomewa sana; ndivyo yalivyo maneno yao walio wakuu wa makusanyiko [“mikusanyo ya maneno,” NW], ambayo yatoka kwa mchungaji mmoja.

  • Je, Unatimiza Wajibu Wako Wote kwa Mungu?
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Novemba 15
    • 13. Maneno ya wale ambao wana hekima ya kimungu yanawezaje kuwa kama michokoro, na ni nani walio kama ‘misumari inayogongomewa sana’?

      13 Maneno ya wale wenye hekima ya kimungu huwa kama michokoro. Kwa njia gani? Hayo huwachochea wasomaji au wasikilizaji wafanye maendeleo kwa kupatana na maneno yenye hekima yanayosomwa au kusikizwa. Pia wale ambao wanajishughulisha mno na “mikusanyo ya maneno,” au maneno ambayo kwa kweli ni yenye hekima na yanafaa, ni kama ‘misumari inayogongomewa sana,’ au inayopigiliwa kabisa. Huenda ikawa hivyo kwa sababu maneno mema ya watu hao yanaonyesha hekima ya Yehova na basi yanaweza kuwategemeza wasomaji au wasikilizaji na kuwafanya wawe thabiti. Ikiwa wewe ni mzazi anayemcha Mungu, je, hupaswi kufanya jitihada nyingi za kukazia kikiki hekima kama hiyo katika akili na moyo wa mtoto wako?—Kumbukumbu la Torati 6:4-9.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki