Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mungu Yumo Katika Hekalu Lake Takatifu
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 17. Isaya arejezea nini aulizapo, “hata lini?”

      17 Isaya ahangaika: “Ndipo nilipouliza, Ee Bwana, hata lini? Naye akanijibu, Hata miji itakapokuwa ukiwa, haina wenyeji, na nyumba zitakapokuwa hazina watu, na nchi hii itakapokuwa ganjo kabisa;

  • Mungu Yumo Katika Hekalu Lake Takatifu
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Isaya 6:11,

  • Mungu Yumo Katika Hekalu Lake Takatifu
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Kwa kuuliza, “hata lini?” Isaya hamaanishi atawahubiria watu wasioitikia hata lini. Badala yake, awahangaikia watu naye auliza hali yao mbaya ya kiroho itaendelea hata lini na jina la Yehova litavunjiwa heshima duniani hata lini. (Ona Zaburi 74:9-11.) Hivyo basi, hali hiyo ya kipumbavu itaendelea hata lini?

      18. Hali mbaya ya kiroho ya watu itaendelea hata lini, na je, Isaya ataishi hata aone utimizo kamili wa unabii huo?

      18 Salala! Jibu la Yehova laonyesha kuwa hali mbaya ya kiroho ya watu hao itaendelea hata matokeo kamili ya kutomtii Mungu yatimizwe, kama yalivyotaarifiwa katika agano lake. (Mambo ya Walawi 26:21-33; Kumbukumbu la Torati 28:49-68) Taifa litaharibiwa, watu watahamishwa, na nchi itabaki ukiwa. Isaya hataishi hata aone jeshi la Wababiloni likiharibu Yerusalemu na hekalu lake mwaka wa 607 K.W.K., ingawa atatoa unabii kwa zaidi ya miaka 40, akiendelea hadi katika utawala wa Hezekia, kitukuu wa Mfalme Uzia. Ijapokuwa hivyo, Isaya atatimiza kwa uaminifu utume wake hadi afapo, zaidi ya miaka 100 kabla ya kutukia kwa msiba huo wa kitaifa.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki