-
Yehova Awaremba Watu Wake kwa Kuwapa NuruMnara wa Mlinzi—2002 | Julai 1
-
-
13, 14. Ni nini kinachoonekana kikija kutoka upande wa magharibi?
13 Sasa geuka utazame upande wa magharibi. Unaona nini? Kule mbali kuna wingu jeupe linaloonekana kana kwamba linafunika uso wa bahari. Yehova anauliza swali ambalo unataka kuuliza: “Ni nani hawa warukao kama wingu, na kama njiwa waendao madirishani kwao?” (Isaya 60:8) Yehova anajibu swali lake mwenyewe:
-
-
Yehova Awaremba Watu Wake kwa Kuwapa NuruMnara wa Mlinzi—2002 | Julai 1
-
-
14 Je, unaweza kuwazia jambo hilo? Lile wingu jeupe limekaribia zaidi na sasa linaonekana kama madoa mengi kule mbali upande wa magharibi. Madoa hayo yanaonekana kama ndege wanaoruka juu tu ya mawimbi ya bahari. Lakini yanapokaribia zaidi, unaona kwamba kumbe ni merikebu zenye matanga yaliyofunguliwa. Merikebu zinazosafiri kuelekea Yerusalemu ni nyingi sana hivi kwamba zinaonekana kama kundi la njiwa. Kundi hilo la merikebu limetoka bandari za mbali na linasafiri kwa kasi kuwapeleka waamini hadi Yerusalemu ili wamwabudu Yehova.
-