Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Jina Jipya”
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • ‘Yehova Amekufurahia’

      9. Eleza jinsi hali ya Sayuni inavyogeuzwa.

      9 Upaji wa jina jipya ni sehemu ya kumgeuza Sayuni wa kimbingu, anayewakilishwa na watoto wake wa kidunia, ili awe na hali ya kupendeza. Tunasoma hivi: “Hutaitwa tena Aliyeachwa, wala nchi yako haitaitwa tena, Ukiwa; bali utaitwa Hefsiba [Namfurahia]; na nchi yako Beula [Ameolewa]; kwa kuwa BWANA anakufurahia, na nchi yako itaolewa.” (Isaya 62:4) Sayuni wa kidunia amekuwa ukiwa tangu alipoharibiwa mwaka wa 607 K.W.K. Hata hivyo, maneno ya Yehova yanamhakikishia kwamba nchi yake itarudishiwa hali yake ya kwanza na kujazwa wakaaji tena. Sayuni aliyeteketezwa wakati mmoja hatakuwa tena mwanamke aliyeachwa pweke, wala nchi yake haitakuwa ukiwa tena. Kurudishwa kwa Yerusalemu mwaka wa 537 K.W.K. kunamaanisha kwamba atapata hali mpya, inayotofautiana kabisa na hali yake ya kwanza ya kuwa magofu. Yehova anatangaza kwamba Sayuni ataitwa “Namfurahia,” na nchi yake itaitwa “Ameolewa.”—Isaya 54:1, 5, 6; 66:8; Yeremia 23:5-8; 30:17; Wagalatia 4:27-31.

      10. (a) Hali ya Israeli wa Mungu iligeuzwaje? (b) “Nchi” ya Israeli wa Mungu ni nini?

      10 Kuanzia mwaka wa 1919 badiliko kama hilo lilipata Israeli wa Mungu. Wakati wa vita ya ulimwengu ya kwanza, Wakristo watiwa-mafuta walionekana ni kama wamekataliwa na Mungu. Lakini mwaka wa 1919 walirudishiwa hali ya kukubalika, na njia yao ya kuabudu ikatakaswa. Jambo hilo liligeuza mafundisho yao, tengenezo lao, na utendaji wao. Taifa la Israeli wa Mungu liliingia katika “nchi” yake, miliki yake ya kiroho, au makao ya utendaji.—Isaya 66:7, 8, 20-22.

  • “Jina Jipya”
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • [Picha katika ukurasa wa 339]

      Yehova atamwita Sayuni wa kimbingu kwa jina jipya

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki