Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Na Tunyoshe Mambo”
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 9, 10. Usafi ni muhimu kadiri gani katika ibada yetu kwa Yehova?

      9 Yehova, Mungu mwenye huruma, sasa atumia sauti changamfu, yenye kuvutia zaidi. “Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya;

  • “Na Tunyoshe Mambo”
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • (Isaya 1:16,

  • “Na Tunyoshe Mambo”
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Hapa twapata mfululizo wa amri tisa. Za kwanza nne zataja kuondolewa kwa dhambi;

  • “Na Tunyoshe Mambo”
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 10 Sikuzote kuoga na usafi vimekuwa sehemu muhimu ya ibada safi. (Kutoka 19:10, 11; 30:20; 2 Wakorintho 7:1) Lakini Yehova ataka usafi upenye ndani zaidi, ufikie moyo hasa wa waabudu wake. Usafi muhimu zaidi ni ule wa adili na wa kiroho, nao ndio anaourejezea Yehova. Amri mbili za kwanza katika mstari wa 16 si za kurudiwa-rudiwa tu. Mwanasarufi wa Kiebrania adokeza kuwa amri ya kwanza, “jiosheni,” yarejezea hatua ya kwanza ya kujisafisha, ilhali ya pili, “jitakaseni,” yarejezea jitihada yenye kuendelea ya kudumisha usafi huo.

      11. Ili kupambana na dhambi, ni lazima tufanye nini, nasi hatupaswi kamwe kufanya nini?

      11 Hatuwezi kumficha Yehova lolote. (Ayubu 34:22; Mithali 15:3; Waebrania 4:13) Basi amri yake inayosema, “Ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu” ina maana moja tu—kuacha kutenda maovu. Bila shaka, hiyo yamaanisha kuepuka kujaribu kuficha dhambi nzito, kwa sababu kuficha dhambi ni dhambi. Mithali 28:13 yaonya hivi: “Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.”

  • “Na Tunyoshe Mambo”
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 14. Isaya 1:16, 17 hutoa ujumbe gani unaofaa?

      14 Yehova atoa ujumbe ulio thabiti na wenye kufaa kama nini kupitia amri hizo tisa! Nyakati nyingine wale wanaotenda dhambi hujiridhisha kwa kufikiri kwamba hawana uwezo wa kufanya mambo mema. Dhana hizo huvunja moyo. Isitoshe, zina makosa. Yehova ajua—naye hutaka tujue—kwamba kwa msaada Wake, mtenda-dhambi yeyote yule aweza kuacha mwendo wake wa dhambi, ageuke kabisa, na badala yake afanye mema.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki