Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Na Tunyoshe Mambo”
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • jifunzeni kutenda mema; takeni [“tafuteni,” “NW”] hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane.” (Isaya 1:16, 17) Hapa twapata mfululizo wa amri tisa.

  • “Na Tunyoshe Mambo”
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • na za mwisho tano zahusu matendo yanayofaa yaongozayo kwenye kupokea baraka ya Yehova.

  • “Na Tunyoshe Mambo”
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 12. (a) Kwa nini ni muhimu ‘kujifunza kutenda mema’? (b) Wazee hasa wanaweza kutumiaje mielekezo inayohusu ‘kutafuta haki’ na ‘kumnyosha anayeonea’?

      12 Kuna mengi ya kujifunza kutokana na matendo mema anayoamuru Yehova hapa katika mstari wa 17 wa Isaya sura ya 1. Ona kwamba hasemi tu “tendeni mema” bali “jifunzeni kutenda mema.” (Italiki ni zetu.) Yahitaji mtu ajifunze Neno la Mungu kibinafsi ili aelewe lililo jema machoni pa Mungu naye atake kulifanya. Na zaidi, Yehova hasemi tu ‘tendeni hukumu na haki’ bali ‘tafuteni hukumu na haki.’ Hata wazee wenye uzoefu wahitaji kutafuta kikamili katika Neno la Mungu ili wapate mwongozo ufaao kwa habari zinazotatanisha. Wao pia wana daraka la ‘kuwasaidia walioonewa [“kuwanyosha wanaoonea,” NW],’ kama Yehova anavyofuatisha kuamuru. Mielekezo hii ni muhimu kwa wachungaji Wakristo leo, kwa kuwa wanataka kulilinda kundi dhidi ya “mbwa-mwitu wenye kuonea.”—Matendo 20:28-30.

      13. Sisi leo twaweza kutimizaje amri zinazohusu yatima na mjane?

      13 Amri mbili za mwisho zahusu baadhi ya watu wa Mungu wasio na ulinzi—mayatima na wajane. Mara nyingi ulimwengu huwadanganya watu kama hao; haipaswi kuwa hivyo miongoni mwa watu wa Mungu. Wazee wenye upendo ‘huwapatia haki’ wavulana na wasichana kutanikoni wasio na baba, wakiwasaidia kupata haki na ulinzi katika ulimwengu unaotaka kuwadanganya na kuwafisidi. Wazee ‘hutetea’ mjane au, kama neno la Kiebrania liwezavyo kumaanisha, “hujitahidi” kwa niaba yake. Kwa kweli, Wakristo wote wahitaji kuandaa ulinzi, faraja, na haki kwa maskini walio miongoni mwetu kwa sababu ni wenye thamani kwa Yehova.—Mika 6:8; Yakobo 1:27.

  • “Na Tunyoshe Mambo”
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 14. Isaya 1:16, 17 hutoa ujumbe gani unaofaa?

      14 Yehova atoa ujumbe ulio thabiti na wenye kufaa kama nini kupitia amri hizo tisa! Nyakati nyingine wale wanaotenda dhambi hujiridhisha kwa kufikiri kwamba hawana uwezo wa kufanya mambo mema. Dhana hizo huvunja moyo. Isitoshe, zina makosa. Yehova ajua—naye hutaka tujue—kwamba kwa msaada Wake, mtenda-dhambi yeyote yule aweza kuacha mwendo wake wa dhambi, ageuke kabisa, na badala yake afanye mema.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki