-
Wokovu na Kushangilia Chini ya Utawala wa MesiyaUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
10, 11. (a) Yesu huwarekebishaje wafuasi wake? (b) Yesu huwapa waovu hukumu gani?
10 Je, sifa bora zaidi za Mesiya zitaathirije hukumu zake? Isaya aeleza: “Kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya.
-
-
Wokovu na Kushangilia Chini ya Utawala wa MesiyaUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
11 Wafuasi wake wanapohitaji kurekebishwa, Yesu huwarekebisha kwa njia inayowanufaisha zaidi—kielelezo bora kwa wazee Wakristo. Kwa upande mwingine, wale wanaozoea uovu wanatarajia hukumu kali. Mungu atakapouhukumu mfumo huu wa mambo, Mesiya “ataipiga dunia” kwa sauti yake yenye mamlaka, huku akitoa hukumu ya kuharibu waovu wote. (Zaburi 2:9; linganisha Ufunuo 19:15.) Hatimaye, hakutabaki watu wowote waovu wanaoharibu amani ya wanadamu. (Zaburi 37:10, 11)
-