-
“Na Tunyoshe Mambo”Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Wakuu wako ni waasi, na rafiki za wevi; kila mtu hupenda rushwa, hufuata malipo; hawampatii yatima haki yake, wala maneno ya mjane hayawawasilii.” (Isaya 1:22, 23)
-
-
“Na Tunyoshe Mambo”Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
22 Mstari wa 23 waonyesha kwa nini ufafanuzi huo wawafaa viongozi hao. Sheria ya Kimusa iliwainua watu wa Mungu, ikiwatenga na mataifa mengine. Kwa kielelezo, ilifanya hivyo kwa kuamuru kulindwa kwa mayatima na wajane. (Kutoka 22:22-24) Lakini katika siku ya Isaya, yatima hana tumaini la kupata hukumu ya haki. Mjane naye hawezi kupata hata mtu wa kusikiliza kesi yake, sembuse mtu wa kujitahidi kwa niaba yake. Hasha, waamuzi na viongozi hawa wanajishughulisha mno na masilahi yao—kutafuta rushwa, kufuata malipo, na kushirikiana na wevi, yamkini kwa kuwalinda wahalifu huku wakiachilia wahasiriwa wateseke. Isitoshe wao ni “waasi,” au wakaidi, katika mwendo wao wa kutenda makosa. Ni hali yenye kuhuzunisha kama nini!
-