Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yehova Anyenyekeza Jiji Lenye Kujigamba
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Chombo cha Mungu cha Kuharibu

      10. Yehova atatumia nani ili kulishinda Babiloni?

      10 Yehova atatumia serikali gani ili kuangusha Babiloni? Miaka ipatayo 200 mapema, Yehova afunua jibu: “Tazama, nitawaamsha Wamedi juu yao, ambao hawaoni fedha kuwa kitu, wala hawafurahii dhahabu.

  • Yehova Anyenyekeza Jiji Lenye Kujigamba
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Isaya 13:17

  • Yehova Anyenyekeza Jiji Lenye Kujigamba
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Yehova atatumia majeshi kutoka nchi ya mbali, yenye milima-milima ya Umedi, ili kuangusha Babiloni lenye utukufu.a

  • Yehova Anyenyekeza Jiji Lenye Kujigamba
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • a Isaya ataja Wamedi peke yao kwa jina, ingawa mataifa kadhaa yataungana dhidi ya Babiloni—Umedi, Uajemi, Elamu, na mataifa mengine yaliyo madogo zaidi. (Yeremia 50:9; 51:24, 27, 28) Mataifa jirani huwaita Wamedi na pia Waajemi kuwa “Mmedi.” Isitoshe, katika siku ya Isaya, Umedi ndiyo serikali kubwa. Uajemi yaja tu kuwa kubwa Koreshi anapotawala.

  • Yehova Anyenyekeza Jiji Lenye Kujigamba
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 11, 12. (a) Umedi yawaje serikali ya ulimwengu? (b) Unabii huo wataja tabia gani isiyo ya kawaida kuhusu majeshi ya Umedi?

      11 Katika siku ya Isaya, Umedi na Babiloni vilevile zatawaliwa na Ashuru. Karne moja hivi baadaye, mwaka wa 632 K.W.K., Umedi na Babiloni zaungana na kupindua Ninawi, jiji kuu la Ashuru. Hatua hiyo yaiwezesha Babiloni kuwa serikali kubwa ya ulimwengu. Yeye hatambui hata kidogo kwamba karibu miaka 100 baadaye, Umedi itamharibu! Ni nani mwingine isipokuwa Yehova Mungu, awezaye kutabiri kwa uhakika hivyo?

      12 Akitambulishapo chombo chake alichokichagua cha kuharibu, Yehova asema kuwa majeshi ya Wamedi “hawaoni fedha kuwa kitu, wala hawafurahii dhahabu.” Ni tabia yenye kushangaza kama nini kwa wanajeshi waliozoea vita! Msomi wa Biblia Albert Barnes asema: “Ni majeshi machache sana yenye kuvamia ambayo hayakuvutiwa na tumaini la kupata nyara.” Je, majeshi ya Umedi yathibitisha kuwa Yehova alisema kweli kwa habari hiyo? Ndiyo. Fikiria maelezo haya yaliyo katika kichapo cha The Bible-Work, kilichoandikwa na J. Glentworth Butler: “Tofauti na mataifa yaliyo mengi ambayo yalipigana vita, Wamedi, na hasa Waajemi, hawakuzingatia sana dhahabu kuliko kupata ushindi na utukufu.”b Kwa hiyo, haishangazi kuwa Koreshi mtawala Mwajemi awaachiliapo Waisraeli kutoka katika uhamisho Babiloni, awarudishia maelfu ya vyombo vya dhahabu na fedha ambavyo Nebukadreza alipora kutoka katika hekalu la Yerusalemu.—Ezra 1:7-11.

      13, 14. (a) Ingawa askari wa Umedi na Uajemi hawatamani nyara, wao watamani nini? (b) Koreshi ashindaje kinga za kujivunia za Babiloni?

      13 Ingawa askari wa Umedi na Uajemi hawatamani sana nyara, wanatamani makuu hata hivyo. Hawataki wawe chini ya taifa jingine lolote ulimwenguni. Zaidi ya hayo, Yehova aweka “maangamizi” mioyoni mwao. (Isaya 13:6)

  • Yehova Anyenyekeza Jiji Lenye Kujigamba
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 14 Ngome za Babiloni hazimzuii Koreshi, kiongozi wa majeshi ya Umedi na Uajemi. Usiku wa Oktoba 5/6, 539 K.W.K., aagiza maji ya Mto Frati yaelekezwe kwingine. Maji yapungukapo, wavamizi waingia jijini kimya-kimya, wakitembea ndani ya bonde la mto katika maji yanayowafikia mapajani. Wakazi wa Babiloni wavamiwa ghafula, na Babiloni laanguka. (Danieli 5:30) Yehova Mungu ampulizia Isaya atabiri matukio hayo, hatua inayohakikisha kwamba Yeye ndiye anayeelekeza mambo.

  • Yehova Anyenyekeza Jiji Lenye Kujigamba
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • b Hata hivyo, yaonekana kwamba baadaye Wamedi na Waajemi walipenda sana anasa.—Esta 1:1-7.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki