-
Shauri la Yehova Dhidi ya MataifaUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
17, 18. (a) Baadhi ya watu katika Israeli waitikiaje ufunuo mbalimbali wa Yehova, lakini itikio la jumla ni nini? (b) Matukio ya leo yafananaje na yale ya siku ya Hezekia?
17 Isaya sasa asema: “Katika siku hiyo mwanadamu atamwangalia Muumba wake, na macho yake yatamtazama Mtakatifu wa Israeli. Wala hataziangalia madhabahu, kazi ya mikono yake; wala hatavitazama vilivyofanyika kwa vidole vyake, maashera na sanamu za jua.” (Isaya 17:7, 8) Naam, baadhi ya watu katika Israeli watii ufunuo wa Yehova wenye onyo. Kwa kielelezo, Hezekia aalikapo wakazi wa Israeli waungane na Yuda kusherehekea Sikukuu ya Kupitwa, Waisraeli fulani wakubali na kusafiri kwenda kusini kuungana na ndugu zao katika ibada safi. (2 Mambo ya Nyakati 30:1-12)
-
-
Shauri la Yehova Dhidi ya MataifaUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
18 Namna gani leo? Israeli lilikuwa taifa lenye kuasi. Basi, jinsi Hezekia alivyojaribu kusaidia watu mmoja-mmoja katika taifa hilo wairudie ibada ya kweli hutukumbusha kuhusu jinsi Wakristo wa kweli leo wanavyojaribu kusaidia watu mmoja-mmoja katika tengenezo lenye kuasi la Jumuiya ya Wakristo. Tangu mwaka wa 1919, wajumbe kutoka katika “Israeli wa Mungu” wameenda kote katika Jumuiya ya Wakristo, wakiwaalika watu washiriki katika ibada safi. (Wagalatia 6:16) Walio wengi wamekataa. Wengi wamewadhihaki wajumbe hao. Ingawa hivyo, baadhi yao wameitikia. Idadi yao sasa imefikia mamilioni, nao hufurahia ‘kumtazama Mtakatifu wa Israeli,’ anayewafundisha. (Isaya 54:13) Wao huachilia mbali ibada kwenye madhabahu zisizo takatifu—ujitoaji na kutumaini miungu iliyotengenezwa na wanadamu—nao kwa hamu humgeukia Yehova. (Zaburi 146:3, 4) Sawa na Mika aliyeishi wakati mmoja na Isaya, kila mmoja wao husema: “Lakini mimi, nitamtazamia BWANA; nitamngojea Mungu wa wokovu wangu; Mungu wangu atanisikia.”—Mika 7:7.
-