Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Shauri la Yehova Dhidi ya Mataifa
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Kuna vita ya wenyewe kwa wenyewe Misri, kukiwa vita ya “mji juu ya mji, na ufalme juu ya ufalme.” (Isaya 19:2, 13, 14) Wanahistoria watoa uthibitisho unaohusu nasaba za wafalme zenye kupambana zikitawala sehemu mbalimbali za nchi hiyo kwa wakati mmoja.

  • Shauri la Yehova Dhidi ya Mataifa
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 27. Ni migawanyiko ipi ya kindani iliyotabiriwa kuhusu “Misri,” na mambo hayo yanatimizwaje leo?

      27 Yehova asema hivi kwa maneno ya unabii kuhusiana na wakati utakaoongoza kwenye kutekelezwa kwa hukumu: “Nitawaamsha Wamisri juu ya Wamisri; nao watapigana, kila mtu na ndugu yake, na kila mtu na jirani yake, mji juu ya mji, na ufalme juu ya ufalme.” (Isaya 19:2) Tangu kusimamishwa kwa Ufalme wa Mungu mwaka wa 1914, “ishara ya kuwapo [kwa Yesu]” imeonekana taifa liinukapo dhidi ya taifa na ufalme dhidi ya ufalme. Mamilioni ya watu katika siku hizi za mwisho wamekufa kwa sababu ya mauaji ya kikabila, maangamizi ya kijamii yenye umwagikaji wa damu, na maangamizi ya watu wa jamii fulani hususa. “Maumivu [hayo] makali ya ghafula ya taabu” hayana budi kuwa mabaya zaidi mwisho ukaribiapo.—Mathayo 24:3, 7, 8.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki