Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yehova Aharibu Kiburi cha Tiro
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • “Toeni Sauti za Uchungu, Enyi Merikebu za Tarshishi”!

      3, 4. (a) Tarshishi ilikuwa wapi, na kulikuwako uhusiano gani baina ya Tiro na Tarshishi? (b) Kwa nini mabaharia wanaofanya biashara na Tarshishi ‘watatoa sauti za uchungu’?

      3 Chini ya kichwa, “Ufunuo juu ya Tiro,” Isaya atangaza: “Toeni sauti za uchungu, enyi merikebu za Tarshishi, kwa maana umeharibika kabisa, hata hapana nyumba, hapana mahali pa kuingia.” (Isaya 23:1a) Yaaminika kwamba Tarshishi ilikuwa sehemu ya Hispania, mbali sana kutoka Tiro iliyo upande wa Mediterania ya mashariki.a Licha ya hayo, Wafoinike walikuwa mabaharia hodari, na meli zao zilikuwa kubwa na bora. Wanahistoria fulani huamini kwamba Wafoinike walikuwa wa kwanza kutambua uhusiano uliopo baina ya mwezi na kujaa na kupwa kwa maji baharini na pia wa kwanza kutumia astronomia iwaongoze katika safari ya baharini. Basi safari ndefu toka Tiro hadi Tarshishi haikuwa kuzuizi kwao.

      4 Katika siku ya Isaya, Tarshishi ya mbali ni soko muhimu kwa Tiro, labda chanzo kikuu cha mali yake wakati fulani wa historia yake. Hispania ina migodi yenye kujaa fedha, chuma, bati, na madini mengineyo. (Linganisha Yeremia 10:9; Ezekieli 27:12.) “Merikebu za Tarshishi,” ambazo labda ni meli za Tiro zinazofanya biashara na Tarshishi, zitakuwa na sababu nzuri ya ‘kutoa sauti za uchungu,’ zikiombolezea kuharibiwa kwa bandari ya kwao.

      5. Mabaharia wanaokuja kutoka Tarshishi watapata wapi habari za kuanguka kwa Tiro?

      5 Mabaharia walio baharini watapataje habari za kuanguka kwa Tiro? Isaya ajibu: “Toka nchi ya Kitimu wamefunuliwa habari.” (Isaya 23:1b) Labda “nchi ya Kitimu” hurejezea kisiwa cha Saiprasi, kilichoko karibu kilometa 100 magharibi mwa pwani ya Foinike. Hicho ndicho kituo cha mwisho kwa meli zinazoelekea mashariki kutoka Tarshishi kabla hazijafika Tiro. Kwa hiyo, mabaharia watapokea habari za kupinduliwa kwa bandari yao waipendayo watuapo huko Saiprasi. Watashtuka kwelikweli! Kwa huzuni, ‘watatoa sauti za uchungu’ kwa kuvunjika moyo.

  • Yehova Aharibu Kiburi cha Tiro
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • a Wasomi fulani huhusianisha Tarshishi na Sardinia, kisiwa kilichoko Mediterania ya magharibi. Kisiwa cha Sardinia pia kilikuwa mbali kutoka Tiro.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki