Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yehova Ni Mfalme
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 9, 10. (a) Kilimo chatimiza fungu gani katika Israeli? (b) Yamaanisha nini kila mtu ‘kukaa chini ya mzabibu wake na chini ya mtini wake’?

      9 Taifa la Israeli ni jamii ya wakulima. Tangu Waisraeli walipoingia katika Bara Lililoahidiwa, wameanza maisha ya ukulima na ufugaji. Basi, sehemu kubwa ya sheria zilizotolewa kwa Israeli yahusu kilimo. Amri yatolewa kuhusu pumziko la sabato kwa nchi kila mwaka wa saba ili rutuba ipate kurejea udongoni. (Kutoka 23:10, 11; Mambo ya Walawi 25:3-7) Misherehekeo mitatu ya kila mwaka ambayo taifa laamriwa kusherehekea yaratibiwa kufungamana na misimu ya kilimo.—Kutoka 23:14-16.

      10 Mashamba ya mizabibu yamejaa nchini mwote. Maandiko huonyesha divai, zao la mzabibu, kuwa zawadi kutoka kwa Mungu ‘inayomfurahisha mtu moyo wake.’ (Zaburi 104:15) Kila mtu ‘kukaa chini ya mzabibu wake na chini ya mtini wake,’ humaanisha kuna ufanisi, amani, na usalama chini ya utawala mwadilifu wa Mungu. (1 Wafalme 4:25; Mika 4:4) Msimu mwema wa divai huonwa kuwa baraka nao ni chanzo cha kuimba na kufurahi. (Waamuzi 9:27; Yeremia 25:30) Kama sivyo mambo ni kinyume. Mizabibu inaponyauka au kukosa kuzaa zabibu na mashamba ya mizabibu yanapogeuka kuwa na mimea ovyo ya miiba, ni uthibitisho kwamba Yehova ameiondoa baraka yake—wakati wa huzuni kubwa.

      11, 12. (a) Isaya atumiaje mashamba ya mizabibu na mazao yake kutoa kielezi cha hali zitakazotokana na hukumu ya Yehova? (b) Isaya afafanua matazamio gani yenye huzuni?

      11 Kwa kufaa basi, Isaya atumia mashamba ya mizabibu na mazao yake kutoa kielezi cha hali zinazotokana na kuondolewa kwa baraka ya Yehova nchini: “Divai mpya inaomboleza, mzabibu umedhoofika, watu wote waliochangamka moyo wanaugua.

  • Yehova Ni Mfalme
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Isaya 24:7

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki