-
Yehova Ni MfalmeUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
13, 14. (a) Yehova ametoa sheria zipi zinazohusu kuvuna? (b) Isaya atumiaje sheria zinazohusu kuvuna ili kutoa kielezi kwamba watu fulani wataokoka hukumu ya Yehova? (c) Ingawa misimu yenye huzuni ya majaribu inakuja, Wayudea waaminifu waweza kuwa na uhakika gani?
13 Wanapovuna zeituni, Waisraeli hupiga miti kwa fito ndipo matunda yaanguke. Kulingana na Sheria ya Mungu, hawaruhusiwi kupanda matawi ya miti ili kuvuna zeituni zilizobakia. Wala hawapaswi kukusanya zabibu zilizobaki baada ya kuvuna mashamba yao ya mizabibu. Mabaki ya mavuno yapasa kuachiwa maskini—ili “mgeni, na yatima, na mjane”—wayaokote. (Kumbukumbu la Torati 24:19-21) Kwa kutumia sheria hizo zinazojulikana vema, Isaya atoa kielezi cha jambo linalofariji kwamba kutakuwapo watakaookoka hukumu ya Yehova inayokuja: “Maana katikati ya dunia, katikati ya mataifa, itakuwa hivi; kama wakati utikiswapo mzeituni, kama wakati waokotapo zabibu baada ya mavuno yake.
-
-
Yehova Ni MfalmeUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
14 Kama vile matunda fulani hubaki mtini au kwenye mzabibu baada ya mavuno, vivyo hivyo kutakuwapo watu fulani watakaobaki baada ya Yehova kutekeleza hukumu yake—“waokotapo zabibu baada ya mavuno yake.” Kama ilivyorekodiwa kwenye mstari wa 6, tayari nabii amewataja, akisema “watu waliosalia wakawa wachache tu.” Lakini, hata kama ni wachache, kutakuwapo watakaookoka uharibifu wa Yerusalemu na Yuda, na baadaye mabaki watarudi kutoka utekwani ili kuijaza nchi tena. (Isaya 4:2, 3; 14:1-5)
-
-
Yehova Ni MfalmeUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
[Picha katika ukurasa wa 265]
Watu fulani wataokoka hukumu ya Yehova, kama vile matunda yanavyobaki mtini baada ya mavuno
-